Jeshi la Polisi nchini kupitia msemaji wake, DCP David Misime, limesema limejipanga kikamilifu kudhibiti uhalifu na kulinda amani kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza na chombo kimoja cha habari leo Oktoba 10, 2025 Misime amesisitiza matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, akionya dhidi ya kusambaza taarifa za uongo, chuki na uchochezi, akisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaokiuka.
Misime amewahakikishia Watanzania kuwa nchi ipo salama na jeshi la oolisi limeimarisha ulinzi kwa raia na mali zao.
Aidha, alibainisha kuwa, zaidi ya askari 3,900 wamesambazwa Tanzania Bara na 388 Zanzibar kutoa elimu ya amani na matumizi bora ya mitandao.
#AzamTVUpdates