Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, ameahidi kuwa endapo chama chake kitaingia madarakani, kitajikita katika kukuza uchumi wa nchi na kuongeza pato la wananchi.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika Handeni, mkoani Tanga, Profesa Lipumba amesema CUF itatekeleza sera madhubuti zitakazoboresha maisha ya Watanzania kwa kuimarisha uchumi na kutoa fursa sawa kwa wote.
Amesisitiza kuwa chama hicho kinalenga kujenga taifa lenye maendeleo jumuishi na ustawi wa wananchi wote.
✍ Mariam Shedafa
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates