Kampeni za uchaguzi zinakaribia kumalizika nchini Cameroon. Wakati takriban wapiga kura milioni 8 wakiwa wameratibiwa kumpigia kura rais wao Jumapili, Oktoba 12, nini matarajio yao siku mbili kabla ya uchaguzi? RFI inakuletea makala maalumu kutoka Yaoundé leo Ijumaa, Oktoba 10, kuanzia 8:10 saa za Afrika ya Kati.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko Douala, Amélie Tulet

Kampeni za ucjhaguzi wa urais nchini Cameroon zimeingia katika hatua yake ya mwisho. Katika siku mbili, Jumapili, Oktoba 12, ingawa wagombea wawili wametangaza kujiondoa kwa kumuunga mkono mwingine—katika kesi hii, Bello Bouba Maïgari—kutakuwa na wagombea rasmi 12 watakaochuana katika uchaguzi ambao Paul Biya, mkuu wa nchi aliye madarakani, ambaye sasa ana umri wa miaka 92, atawania muhula wa nane baada ya miaka 43 madarakani.

Huku kukiwa na takriban wapiga kura milioni 8 waliojiandikisha kupiga kura, kulingana na Elécam, tume ya uchaguzi ya Cameroon, ni nini matarajio, hofu na matumaini yao katika mkesha wa uchaguzi?

“Nimechoshwa, nina hamu ya mabadiliko. Mambo hayaendi sawa, serikali inahitaji kubadilika,” anasema Adéran, mwanafunzi anayejiandaa kupiga kura kwa mara ya kwanza. Akiwa amezungukwa na watihimu wasio na ajira, ana hamu ya kupiga kura.

“Sidhani kama mabadiliko yanatokana na kupiga kura”

Katika chuo kihuu hicho hicho, Flavien hakuweza kuchukua kadi yake ya wapiga kura na anakakata tamaa: “Sioni mabadiliko yoyote kwa Wacameroon katika uchaguzi huu,” analalamika, huku akiungwa mkono na Bertin, mwalimu, ambaye pia haamini katika zoezi hili la kiraia: “Sidhani mabadiliko yanatokana na upigaji kura,” anasisitiza, ingawa atapiga kura bila kujali: “Hata tone la mvua ndani ya bahari, bado ni tone tu. kura yangu itakuwa na athari, lakini lazima nifanye hivyo, ni hivyo tu,” ameongeza.

Wakati Olivier pia anajitahidi kuamini mchakato huo, Johnson, kinyume chake, anaonyesha kujiamini – “Nina ujasiri sana: ni nchi yangu!” anasema – wakati Raymond anatumai kuona aina fulani ya mwendelezo: “Ninachotaka ni amani, kwa hivyo nitapigia kura CPDM [chama tawala] kwa utulivu,” anasema.

Kuhusu Michèle, ambaye ameamua kupiga kura kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 38, anatumai kwamba kila kitu kitafanywa ili kuhakikisha uaminifu wa uchaguzi huo. “Ninahofia kutakuwa na udanganyifu zaidi, kutakuwa na wizi wa kura. Ni lazima uchaguzi ufanyike kwa uwazi na matokeo yake lazima yaakisi kwa usahihi matakwa ya raia wa Cameroon,” anasema, ingawa Élécam imetangaza kujitolea kwake kuandaa uchaguzi wa amani, ulio wazi, usio na upendeleo na jumuishi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *