
Serikali ya Israel imetangaza leo Ijumaa, Oktoba 10, kwamba imeidhinisha makubaliano ya kuwaachilia mateka huko Gaza, hatua mpya katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano huko Gaza na kuachiliwa kwa mateka iliyotiwa saini Alhamisi na Hamas, chini ya mwamvuli wa Marekani.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Makubaliano yaliyofikiwa nchini Misri ni sehemu ya mpango wa amani wenye pointi 20 kwa Gaza, kufuatia miaka miwili ya vita vya vibaya vilivyochochewa na shambulio lisilokuwa na kifani la Hamas dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7, 2023. Wanajeshi mia mbili wa Marekani watatumwa “kusimamia” na “kutazama” utekelezaji wa makubaliano kuhusu Gaza.
Serikali ya Israel imeidhinisha awamu ya kwanza ya mpango wa amani wa Gaza, unaotoa usitishaji mapigano na kurejea kwa mateka wa Israel na wafungwa 2,000 wa Kipalestina. Serikali ya Israel kusaini makubaliano hayo kunafungua njia ya kusitishwa kwa vita ndani ya saa 24 na kuachiliwa kwa mateka ndani ya saa 72.
“Serikali imeidhinisha tu mfumo wa kuachiliwa kwa mateka wote – walio hai au waliofariki,” ofisi ya serikali ya Israel imesema, na kuruhusu makubaliano hayo kuanza kutekelezwa.
Mrengo wa kulia unakataa makubaliano hayo, ambayo yanatoa fursa ya kuachiliwa kwa wafungwa 2,000 wa Kipalestina, lakini hautaki kuondoka kwenye muungano huo katika hatua hii.
Makubaliano haya, yaliyofikiwa usiku wa jana kuamkia leo Ijumaa nchini Misri, ni sehemu ya mpango wa amani wenye pointi 20 kwa Gaza uliotangazwa Septemba 29 na Rais wa Marekani Donald Trump, baada ya miaka miwili ya vita vya kutisha vilivyochochewa na shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa la vuguvugu la Kiislamu la Palestina Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba 2023.
Kati ya watu 251 waliotekwa nyara na kupelekwa Gaza siku hiyo, 47 bado wanazuiliwa huko, angalau 25 kati yao walifariki, kulingana na jeshi. Mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Israel yamesababisha makumi ya maelfu kuuawa na kusababisha maafa ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza.
Kabla ya kuidhinishwa na serikali, makubaliano hayo yaliidhinishwa na baraza la usalama la Israel. Waziri wa Usalama wa Ndani wa Israel kutoka mrengo wa kulia , Itamar Ben Gvir, alipinga hilo.
Wanajeshi mia mbili wa kijeshi wa Marekani watatumwa “kusimamia” na “kutazama” utekelezaji wa makubaliano ya Gaza, afisa mkuu wa Marekani alisema siku ya Alhamisi kwa sharti la kutotajwa.