Jumamosi ya pili ya kila Oktoba dunia huadhimisha ‘Siku ya Tiba Shufaa’ yanayoelezwa kuwasaidia watu wengi waliougua magonjwa ya muda mrefu na yenye maumivu makali ikiwemo saratani huku hapa nchini ikielezwa kuwa bado kuna changamoto ya elimu ya utolewaji wa matibabu hayo.
Ukosefu wa elimu hiyo umewaibua watoaji wa huduma hiyo kutumia jukwaa la maadhimisho ya siku hiyo kutoa elimu ya matibabu hayo ambayo pia inatolewa pia katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Sheila Mkumba amezungumza na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Tiba wa Wizara ya Afya, Dkt. Mwinyikondo Amir, Mwenyekiti wa Chama Cha Watoa Tiba Shufaa (TPCA), Dkt. Hussein Mtiro na Dkt. Asafil Munena ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ocean Road.
Pia Sheila amezungumza na shujaa wa saratani ya matiti, Jasmine Said.
Mhariri @moseskwindi