Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, HAMAS pamoja na makundi mengine washirika ya Muqawama wa Palestina yamesisitiza kuwa uamuzi wowote kuhusu utawala wa baadaye wa Ghaza ni “suala la ndani la Palestina” na kupinga vikali eneo hilo kutawaliwa na kusimamiwa na maajinabi.

Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa jana Ijumaa na harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina (PIJ) na ya Wananchi kwa ajili ya Ukombozi wa Palestina (PFLP), makundi hayo ya Muqawama yaliungana na Hamas katika kupongeza istiqama na Muqawama wa Wapalestina, ambao yamesema, ulivuruga mipango na njama za utawaIa wa kizayuni wa Israel ya kuwalazimisha wayahame makazi yao huko Ghaza.

“Tunasisitiza upya kukataa kwetu usimamizi wowote wa kigeni, na tunasisitiza kwamba asili ya vipi utawala wa Ukanda wa Ghaza na taasisi zake uwe ni suala la ndani la Palestina la kuamuliwa moja kwa moja na watu wetu kitaifa”, imesema taarifa hiyo.

Makundi hayo ya Muqawama wa Palestina yameongeza kuwa yamo mbioni kuandaa “mkutano wa dharura wa kitaifa” kujadili hatua zitakazofuata baada ya kusitishwa mapigano.

“Hii itaunganisha msimamo wa Palestina, kuunda mkakati wa kitaifa wa kina, na kujenga upya taasisi zetu za kitaifa kwa misingi ya ushirikiano, uaminifu, na uwazi,” yamesisitiza makundi hayo katika taarifa yao.

Bado haijafahamika kama mrengo wa Fat-h unaoshikilia hatamu za uongozi wa Mamlaka ya Palestina umekubali kuwa sehemu ya mkutano huo au la.

Mpango wa vipengele 20 uliopendekezwa na Rais wa Marekani Donald Trump kwa ajili ya Ghaza unajumuisha kuundwa chombo kipya cha kimataifa, kilichopewa jina la “Bodi ya Amani”, ambacho kitakuwa na jukumu la kusimamia mamlaka ya muda ya wateknokrati ya kuitawala Ghaza.

Kwa mujibu wa mpango huo, Trump mwenyewe amepangwa kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo, itakayomjumuisha pia waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *