#HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Arusha linawashikilia watu watano wanaotuhumiwa kuhusika katika mauaji ya Omary Mnandi, mwenye umri wa miaka 30, ambaye alikuwa askari polisi mkazi wa Jiji la Arusha.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, ametoa taarifa hiyo leo Oktoba 12, 2025, akieleza kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo usiku wa Oktoba 11, 2025, katika Bar inayojulikana kama Simaloi iliyopo katika eneo la Kaloleni.
Kamanda Masejo amefafanua kuwa watuhumiwa hao walimjeruhi Omary Mnandi katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hali ambayo ilisababisha kifo chake wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru, Arusha.
Amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni baada ya askari polisi huyo, Omary Mnandi, kutokana na unywaji wa pombe, kukosea uhakika wa gari lake namba T. 402 CNC, na hivyo kuingia kwenye gari namba T. 734 AXR la mmoja wa watuhumiwa hao, na ndipo walipoanza kumshambulia.