#HABARI: Serikali wilayani Kakonko mkoani Kigoma, imepiga hatua katika masomo ya Sayansi hasa kwa wanafunzi wa kike baada ya kuanzisha shule ya sekondari ya wasichana na kusaidia kunusuru wasichana wengi waliokuwa wakimaliza shule ya msingi na Kwenda kutumikishwa kazi za ndani katika mikoa mbali mbali na wengine kupewa ujauzito na hivyo kushindwa kutimiza malengo yao.

Akizungumza wakati wa ziara ya Mkuu wa mkoa wa Kigoma Simon Sirro , katika Wilaya ya Kakonko Mkuu wa Wilaya hiyo Kanali Evance Mallasa, amesema kuwa ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana Kakonko ni mkombozi kwa wasichana wilayani humo huku mkurugenzi wa halimashauri ya wilaya ya Kakonko Stephano Ndaki akieleza mikakati iliyowekwa katika kuhakikisha wasichana wanatimiza ndoto zao.

Naye Mkuu wa mkoa wa Kigoma Balozi Mstaafu Simon Sirro, amewapongeza viongozi wa wilaya ya Kakonko kwa ubunifu huo na kuwataka viongozi katika wilaya nyingine za mkoa huo kufika wilayani kakonko kwa ajiri ya kujifunza ili kuwakomboa Watoto wa kike na matatizo mbali mbali ambayo yanasababisha kushindwa kufikia malengo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *