Baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela mnamo Septemba 25, 2025, kwa ufadhili wa Libya wa kampeni yake ya 2007, rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy atajua tarehe na masharti ya kifungo chake leo Jumatatu hii, Oktoba 13.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kuanza kutumikia kifungo chake  inakaribia. Kwa mara ya kwanza, rais wa zamani wa nchi mwanachama wa Umoja wa Ulaya atafungwa jela. Leo Jumatatu, Oktoba 13, Nicolas Sarkozy ameitwa na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa taifa inayoshughulikia masuala ya Fedha, ambayo itamjulisha tarehe na masharti ya kuzuiliwa kwake.

Mnamo Septemba 25, Mahakama ya Paris ilimhukumu kifungo cha miaka mitano jela, miaka mitano ya kutostahiki, na faini ya Euro 100,000 katika kesi ya ufadhili wa Libya katika kampeni yake ya uchaguzi wa urais wa 2007. Majaji walimkuta na hatia ya njama ya uhalifu kwa kuwaruhusu washirika wake wa karibu kwenda nchini Libya wakati wa utawala wa Muammar Gaddafi kwa nia ya kupata kufadhili wa kampeni yake ya uchaguzi kinyume cha sheria.

Ingawa amekata rufaa dhidi ya hatia yake, rais huyo wa zamani hataweza kukwepa jela, kwa kuwa hukumu iliyotolewa inaambatana na agizo la dhamanalinalotaka umuzi wa mahaka uanze kutekelezwa. Katika hukumu yake, mahakama ilihalalisha hili kwa “mvuto wa kipekee wa vitendo” vilivyofanywa na bingwa wa zamani wa mrengo wa kulia.

Rais huyo wa zamani wa Ufaransa, kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2012, huenda akafungwa jela baada ya kuitishwa na ofisi ya mwendesha mashitaka leo Jumatatu. Hata hivyo, wangeweza kumpa siku chache za ziada ili kujitayarisha kwa ajili ya kuwekwa kizuizini. Uwezekano huu umetolewa na Kanuni ya Ufaransa ya Utaratibu wa Jinai, ambayo inasema kwamba “tarehe ya kufungwa imedhamiriwa kwa kuzingatia hali ya kibinafsi ya mtu aliyehukumiwa […].” Kuwekwa kwake katika jela kutafanyika “hivi karibuni,” chanzo kimeliambia shirika la habari la Agence France Presse (AFP) wakati wa hukumu.

Kwa hali yoyote, muda huu wa kifungo hauwezi kuzidi miezi minne baada ya mkutano na majaji. Hii ina maana kwamba Nicolas Sarkozy atafungwa kabla ya Februari 13, 2026.

Kifungo cha upweke?

Ingawa Nicolas Sarkozy ni mshtakiwa kama mtu mwingine yeyote, hata hivyo ni Rais wa zamani wa Jamhuri. Hii inamaanisha marekebisho kadhaa kutoka kwa mtazamo wa kuzuiliwa kwake. Ili kuhakikisha usalama wake, mkuu huyo wa zamani wa nchi anaweza kufungwa katika sehemu ya “watu walio katika mazingira magumu”, iliyotengwa kwa ajili ya wafungwa nyeti, kama vile wanasiasa au wanahabari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *