Wakati macho yote yakielekezwa Mashariki ya Kati, Ukraine inaendelea kushambuliwa kila siku na Urusi, na Rais Volodymyr Zelensky anaonya kuhusu hali mbaya ambayo nchi hiyo inapitia kwa sasa.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Vita vya Urusi dhidi ya Ukraine bado vinaendelea kushika kazi kwenye mstari wa mbele, na katika hotuba yake ya kila siku, Volodymyr Zelensky anakariri matarajio ya Kyiv kwa washirika wake, hasa Marekani. Wakati rais wa Ukraine aanakiri kwamba amezungumza mara mbili ndani ya siku mbili na mwenzake, Donald Trump, anabainisha haja ya Ukraine ya ulinzi wa anga wakati nchi hiyo inakumbwa na kampeni mpya ya mashambulizi makubwa sio tu kwenye miundombinu yake ya nishati, umeme na gesi, lakini pia kwenye mtandao wake wa reli, anaripoti mwandishi wetu huko Kyiv, Emmanuelle Chaze.

Urusi inatumia fursa ya hali ya sasa – huko Mashariki ya Kati na matatizo ya ndani katika kila nchi yanavutia umakini wa hali ya juu. Mashambulizi ya Urusi yamekuwa ya kudharauliwa zaidi,” ameonya.

Uwezekano wa uwasilishaji wa makombora ya masafa marefu ya Marekani ya Tomahawk uliibuliwa hivi karibuni na maafisa wa Marekani, na kuibua hasira ya Moscow. Kiongozi wa Ukraine hakutaja siku ya Jumapili iwapo aliomba makombora hayo, akisema tu: “Tunaona na kusikia kwamba Urusi inaogopa kwamba Marekani inaweza kutupa Tomahawks, ambayo ni ishara kwamba shinikizo kama hilo linaweza kufanya kazi kwa amani.”

“Mgogoro mpya” kwa mujibu wa Putin

Mapema mwezi Oktoba, Vladimir Putin alionya kwamba kutuma silaha hizi kwa Kyiv kungechochea “uhasama mpya” kati ya Moscow na Washington kwa sababu “kutumia Tomahawks haiwezekani bila ushiriki wa moja kwa moja wa wanajeshi wa Marekani.” Urusi hata hivyo inahakikisha kwamba kupewa makombora ya Tomahawks hakutabadilisha hali katika mstari wa mbele, ambapo vikosi vyake vimekuwa vikisonga mbele kwa mwendo wa kinyonga mashariki mwa Ukraine tangu mwanzo wa mashambulizi ya Urusi mnamo mwezi Februari 2022, kwa gharama ya hasara kubwa.

Volodymyr Zelensky pia ametoa tahadhari kuhusu kukatika kwa mtambo wa nyuklia wa Zaporizhzhia, unaokaliwa kinyume cha sheria na Urusi, ambao kwa wiki tatu zilizopita umekuwa ukitumia jenereta zake za ziada za dizeli.

Kwa upande wa Ulaya, Volodymyr amekutana na Emmanuel Macron. Rais wa Ufaransa amebainisha kwamba ikiwa Moscow itaendelea kukataa mazungumzo, Urusi italazimika kulipa gharama kwa tabia yake ya ukaidi kuhusiana na vita hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *