#HABARI: Idara ya Uhamiaji inapenda kuutarifu Umma kuwa tarehe 13 Oktoba, 2025 imewaondosha
nchini raia wawili wa kigeni ambao ni Dkt. Brinkel Stefanie mwenye hati ya kusafiria ya
Ujerumani namba C475MMNGL na Bi. Catherine Janel Almquist Kinokfu mwenye hati
ya kusafiria ya Marekani namba A80321764 baada ya kubainika kuwa wamekiuka masharti
ya viza zao za matembezi.

Aidha, Idara ya Uhamiaji inatoa wito kwa raia wa kigeni wanaoingia na kuishi nchini kwa
madhumuni mbalimbali kuzingatia matakwa yaliyoainishwa katika viza au vibali vyao kwa
mujibu wa Sheria ya Uhamiaji Sura 54 pamoja na Kanuni zake ili kuepuka usumbufu
unaoweza kujitokeza pindi wanapokiuka sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *