#HABARI: Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na MKA Foundation kwa mara nyingine wamefanikiwa kufanya upasuaji wa kibingwa wa kumtengenezea mgonjwa taya jipya kwa kutumia kipande cha ubavu wake mwenyewe.
Akizungumza baada ya Upasuaji huo Bingwa wa Upasuaji wa Mataya, Uso na Kinywa MNH Dkt. Anold Agostino, amesema upasuaji huo umefanyika kwa mgonjwa ambaye taya lake liliharibiwa kutokana na uvimbe kwenye mataya, uso na kwa ambao wana saratani ya kinywa na meno, hali iliyomsababishia kupoteza sehemu kubwa ya taya. Ili kurejesha umbo la uso na uwezo wa kutafuna, tunachukuwa sehemu ya mifupa ya mgonjwa kutoka kwenye kiuno na mbavu ili kutengeneza taya jipya kwa mgonjwa huyo.
Mafanikio haya yanadhihirisha dhamira ya Serikali kupitia Wizara ya Afya katika kuboresha huduma za ndani ya nchi, kupunguza gharama za matibabu nje, na kuimarisha uwezo wa madaktari wazawa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.