#TANZIA

Azam Media Limited inasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wake, Ally Mkongwe, kilichotokea Novemba 7, 2025 katika Hospitali ya Besta, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mkongwe ambaye alikuwa Mwongoza Matangazo ya televisheni katika Idara ya Uzalishaji Maudhui, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa zaidi ya miezi miwili.

Anatarajiwa kuzikwa Novemba 8, 2025 katika makaburi ya Makoka, Dar es Salaam.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *