
Wanaharakati hao Bob Njiagi na Nicholas Oyoo walikamatwa na watu wenye silaha Oktoba 1, baada ya kuhudhuria mkutano wa kisiasa wa mpinzani mkuu wa Museveni Robert Kyagulani maarufu Bobi Wine. Awali, serikali ya Uganda ilikanusha kuhusika na kukamatwa kwa wanaharakati hao wawili.
Mazungumzo ya kidiplomasia yafanikisha kuwarejesha nyumbani
Waziri wa Mambo ya nje ya Kenya Musalia Mudavadi amesema Njagi na Oyoo walikabidhiwa kwa balozi wa Kenya baada ya wiki kadhaa za mawasiliano yaliyokuwa ya “uwazi na yenye kujenga”. Wanaharakati hao baada ya kutua Kenya Jumamosi, bila maelezo zaidi wamesema walikuwa wakishikiliwa kwenye kambi ya kijeshi katika mazingira yasiyozingatia utu.