Mamlaka za Gaza zimefafanua kuwa, takriban Wapalestina 241 wameuawa na wengine 614 wamejeruhiwa tangu Oktoba 11, siku moja baada ya kuanza kwa utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha vita.

Idadi jumla ya vifo iliyotolewa, inajumuisha miili ya Wapalestina waliorejeshwa Gaza kutoka Israel kama sehemu ya makubaliano hayo.

Mwili wa mwanajeshi waliyeuawa 2014 warejeshwa Israel

Wakati huo huo, Israel imesema imeupokea kupitia shirika la msalaba mwekundu mwili unaodaiwa kuwa wa mwanajeshi Hadar Goldin aliyeuawa mwaka 2014 kutoka kwa wanamgambo wa Hamas. Kama vipimo vya kubaini vinasaba vya DNA, vikithibitisha, mwili huo utakuwa wa 24 kurudishwa Israel tangu makubaliano ya kusitisha vita Gaza yalipoanza kutekelezwa Oktoba 10.

Kulingana na Hamas, mwili wa Goldin ulikutwa kwenye handaki katika mji wa kusini mwa Ukanda wa Gaza wa Rafah jana Jumamosi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *