Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kimepanga kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 12,000 wa sasa hadi kufikia 17,970 baada ya kukamilika kwa majengo mapya katika ndaki kuu ya Mbeya na ndaki ya Rukwa, yaliyogharimu zaidi ya shilingi bilioni 46.3.
Majengo hayo yana uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,500 kwa wakati mmoja katika ndaki kuu ya Mbeya na wanafunzi 2,470 katika ndaki ya Rukwa kuanzia mwaka wa masomo 2025/26.
#AzamTVUpdates
✍Kakuru Msimu
Mhariri | John Mbalamwezi