Afisa wa ngazi za juu wa Uturuki alisema nchi yake imefanikisha kurejeshwa kwa mabaki ya mwili wa Hadar Goldin baada ya juhudi za kina “zinazoakisi dhamira njema ya kundi la Hamas” kwenye mpango wa kusitisha mapigano.

Hata hivyo, afisa huyo aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba kinachofuatia sasa ni kuwahakikishia raia hao walionasa kwenye njia za chini ya ardhi huko Gaza  wanatoka salama.

Hayo yakijiri, kundi la Hamas lilisema wapiganaji wake waliozungukwa kwenye eneo la Rafah linaloshikiliwa na Israel wasingesalimu amri, na badala yake limewataka wapatanishi kusaka suluhisho la mzozo huo unaoweza kuhatarisha usitishaji mapigano. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *