
“Uanzishwaji wa ubalozi wetu huko Vatican utaimarisha uhusiano wetu na taasisi za maendeleo za Kikatoliki ambazo zinaendesha jumla ya shule 7,700 na vituo vya afya 500 nchi nzima,” ilisomeka sehemu ya taarifa ya baraza hilo.
Kulingana na baraza hilo, uwepo wa ofisi ya ubalozi nchini Vatican, ni wa faida kwa Kenya, kutokana na fursa za maendeleo ya miradi ya kijamii kama vile elimu na dini.