
Hannibal alikamatwa mwaka 2015 nchini Syria kutokana na madai ya kuwa na taarifa kuhusu kutoweka kwa kiongozi wa Kiislamu wa Kishia, Imam Musa al-Sadr, ambaye alipotea mwaka 1978 akiwa ziarani Libya.
Wakati huo, Hannibal alikuwa na umri wa miaka miwili pekee, jambo lililowafanya wengi kuhoji uhalali wa kumhusisha na tukio hilo.
Baada ya shinikizo kutoka kwa wanaharakati wa haki za binadamu, mahakama iliamua kupunguza dhamana yake kutoka dola milioni 11 hadi takriban dola 900,000, na baadaye kufuta marufuku ya kusafiri.
“Kuachiliwa kwa Gaddafi kulikuja baada ya mawakili wake kulipa dhamana,” shirika la habari la National News liliripoti.