#HABARI: Jumla ya tani 99,788.659 za Korosho ghafi zimeuzwa katika minada minne ya awali ya msimu wa mauzo wa mwaka 2025/2026, kwa bei ya juu ya shilingi 3,520 na bei ya chini ya shilingi 2,310 kwa kilo, kupitia mfumo wa Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).
Akizungumza leo, Afisa Mtendaji Mkuu wa TMX, Godfrey Malekano, amesema jumla ya Tani 93,879.726 sawa na asilimia 94.1 ya Korosho zote zilizowasilishwa sokoni zimeuzwa huku asilimia 5.9 pekee zikikosa mnunuzi, hali inayoonesha mafanikio makubwa ya mfumo huo wa biashara.
Malekano amesema kiwango hicho cha mauzo ni cha kihistoria katika tasnia ya Korosho, kwani haijawahi kutokea kwa mzigo mkubwa kiasi hicho kuuzwa kwa wakati mmoja tangu kuanzishwa kwa mfumo wa minada kupitia TMX.
Amefafanua kuwa katika minada hiyo, vyama vikuu vya ushirika vimechangia kiasi kikubwa cha korosho zilizouzwa, ambapo MAMCU iliwasilisha sokoni zaidi ya tani 40,000, RUNALI tani 20,000, TANECU tani 26,000, na LIMWAMBAO tani 11,000.
“Matokeo haya yanaonesha ufanisi wa mfumo wa TMX katika kuhakikisha wakulima wanapata soko la uhakika na lenye ushindani wa bei.