#HABARI: Wakulima wa Korosho katika maeneo yanayohudumiwa na Chama Kikuu cha Ushirika cha TANECU LTD, wameelezea furaha na kuridhishwa kwao baada ya chama hicho kufanya malipo ya awali kwa haraka kuliko ilivyozoeleka.
Kwa kawaida, malipo ya Korosho huchukua takribani siku saba au zaidi tangu kufanyika kwa mnada lakini katika msimu huu TANECU imeweka rekodi mpya kwa kuwalipa wakulima ndani ya siku sita tu baada ya kufanyika kwa mnada wa kwanza.
Wakulima kutoka maeneo mbalimbali wamesema hatua hiyo inaonesha dhamira ya chama kuboresha huduma na kuondoa changamoto za ucheleweshaji wa malipo, jambo ambalo hapo awali limekuwa likiwapa usumbufu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.