Jumla ya vijiji 20 vilivyopo katika wilaya nne za mkoa wa Tanga vimenufaika na mradi wa utunzaji wa mazingira ya bahari kupitia vikundi vya Mfuko wa Kutunza Bahari (MKUBA), unaotekelezwa na Shirika la Mwambao Coastal Community Tanzania.

Mbali na wavuvi kupatiwa elimu ya utunzaji wa mazingira ya bahari, pia wamewezeshwa katika vikundi vyao kwa kupatiwa mikopo isiyokuwa na riba, ambapo hadi sasa zaidi ya shilingi milioni 200 tayari zimetoa kuwafikia wanufaika.

✍ Mariam Shedafa
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *