#HABARI: Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amewataka watendaji wa Wizara ya Afya kufanya kazi kwa bidii, weledi na uadilifu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea ili kuleta tija na ufanisi kwa wananchi.
Mhe. Mchengerwa ametoa wito huo alipokutana na Menejimenti ya Wizara mara baada ya kuwasili rasmi kuanza majukumu yake mapya ya kazi kwenye Wizara hiyo.
Amesema huu ni wakati wa watumishi kuongeza juhudi na kutobweteka, ili kuendelea kusukuma maendeleo ya Sekta ya Afya mbele.
Waziri Mchengerwa amewataka watumishi wote kufuata maadili ya kazi na kusimamia kwa umakini maelekezo yanayotolewa, ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.