#HABARI: Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso, ameanza utekelezaji wa mkakati mahsusi wa kuboresha huduma ya maji katika Jiji la Dodoma, kupitia miradi ya muda mfupi yenye thamani ya shilingi Bilioni 62.
Akizungumza na Menejimenti na Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Waziri Aweso amesema pamoja na hatua kubwa zilizokwisha kuchukuliwa na Serikali, Wizara imeandaa mikakati ya muda mfupi, wa kati na mrefu ili kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dodoma na maeneo ya pembezoni.
Waziri Awso amesisitiza dhamira ya Serikali kuendelea kuwekeza rasilimali fedha, nguvu na utaalamu ili kuhakikisha Jiji la Dodoma linakuwa na huduma ya maji ya uhakika.
Kwa upande mwingine, Aweso amesema Wizara itaimarisha eneo la utoaji huduma kwa wateja ili kupunguza kero na malalamiko ya wananchi huku akisisitiza umuhimu wa kufuata Mkataba wa Huduma kwa Mteja.
Hata hivyo, ameitaka Mamlaka za Maji kote nchini kutokuzoea malalamiko ya wananchi na badala yake kuchukua hatua za haraka kutatua changamoto zao pale zinapojitokeza, ikiwa ni pamoja na kuachana na urasimu unaowakwaza wateja.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)