Wahitimu zaidi ya 200 wa ngazi mbalimbali za kozi za kitaaluma za maji wamehakikishiwa nafasi za ajira sambamba na ushirikiano wa kikazi na serikali kupitia wizara ya maji hususani kwenye fursa za utekelezaji wa miradi ya usambazaji maji kwenye maeneo ya vijijini ambayo kwa kiasi kikubwa hayajafikiwa na huduma za maji safi na salama.

Kwa mujibu wa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ushirikiano huo kupitia vikundi rasmi vya wataalamu unatarajia kuhusisha miradi yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 10.

Imeandaliwa na @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *