Wakazi zaidi ya 3000 wa vijiji vya Nangumi na Likonde, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara vijijini wamedai upatikanaji wa maji safi na salama umekuwa kwa kiwango cha chini tangu kuanza kusimamiwa na mamlaka ya maji Mtwara (MTUWASA) tangu mwaka 2019.
Wananchi wa vijiji vya Nangumi na Likonde ni kati ya wakazi wanaonufaika na mradi wa maji wa Mbuo unaozalisha lita million moja na laki saba kwa siku ukihudumia Kata ya Mbuo na Mayanga, kwasasa wananchi wa vijiji hivyo wamelalamikia tatizo hilo la kukosekana kwa maji vijiji mwao.
#AzamTVUpdates
Mhariri | @claud_jm