#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Jabiri Omari Makame amesema kile kilichofanyika wakati na baada ya siku ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania Oktoba 29, 2025 kilikuwa ni fujo, vurugu na njama za kupangwa za kuharibu uchaguzi na kuiangusha Serikali ya Tanzania.

Mhe. Makame amebainisha hayo wakati wa Kikao kazi na watumishi wa Mkoa wa Songwe, akisema amelazimika kueleza hayo kwa wananchi na Watumishi wa mkoa huo ili wafahamu wajibu wao katika kukabiliana na matishio ya amani dhidi ya watu wenye nia ovu na mustakabali wa nchi.

Katika maelezo yake, Mhe. Makame amesema kulingana na mahojiano ya watuhumiwa waliokamatwa kutokana na vurugu hizo, wengi walifuata mikumbo, wengine wakilipwa fedha ili kutekeleza vurugu zile, huku kati yao zaidi ya asilimia 90 ya waratibu, washiriki na wafadhili wa vurugu hizo wakitokana na chama kimoja cha siasa ambacho hakukitaja kwa jina lake.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *