
Nigeria. Baba wa marehemu mwanamuziki Ilerioluwa Aloba “Mohbad”, Joseph Aloba, ameweka wazi kuwa sababu pekee inayochelewesha mazishi ya mwanawe ni kukamilika kwa kipimo cha DNA cha mtoto wa Mohbad.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumanne, Desemba 2, nje ya mahakama kabla ya kesi ya DNA kusikilizwa, Aloba amesema huwenda mazishi ya mwanaye ya kafanyika hivi karibuni baada ya majibu ya kipimo hicho kutoka.
“Leo ni kesi ya DNA mahakamani. Tuko hapa sasa. Wakili wangu yupo. Ninaiambia dunia nzima kwamba hili ndilo jambo muhimu zaidi na ndilo linalochelewesha mazishi ya Mohbad. Baada ya DNA kufanyika, ndipo tunaweza kuendelea na hatua ya mazishi. Ni matumaini yangu haitachukuwa muda sana,”amesema
Mohbad alifariki dunia Septemba 2023 katika mazingira ya kutatanisha huku msiba wake ukitikisa nchi nzima ya Nigeria mashabiki wakiandamana kutaka kujua sababu ya kifo cha msanii huyo.
Hata hivyo moja ya jambo kubwa ni mtoto aliyeachwa na msanii huyo, ambapo Joseph Aloba ameendelea kusisitiza na kutaka uthibitisho kama mtoto huyo ni wa kibaiolojia wa Mohbad.