#HABARI: Kufuatia vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025 kipindi cha Uchanguzi Mkuu na baada ya uchaguzi hali iliyosababisha vifo vya watu na mali za watu binafsi na za umma kuharibiwa, baadhi ya wajumbe wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) wameishauri Serikali wakidai inapaswa kuponya majeraha ya vidonda vya watu wote waliopata athari ya kuondokewa na wapendwa wao pamoja na walioharibikiwa mali zao katika vurugu hizo kabla ya kwenda kwenye maridhiano.

Wamesema hali inaonyesha kuna uwepo wa kundi kubwa la vijana ambalo linaonyesha halijaridhishwa na kilichotokea kwenye vurugu hizo na hawana mahali pakusemea ili kuleta muafaka wa pamoja.

Hayo yamejiri jijini Dodoma mara baada ya jumuiya hiyo kutoa tamko lao lenye hoja kumi na moja kufuatia kadhia iliyotokea siku ya uchaguzi mkuu nchini.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *