CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kwa kauli moja kimeunga mkono hotuba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoitoa Oktoba 3 na kusema kuwa hotuba hiyo inaoonyesha dhamira ya kweli na mwelekeo sahihi wa Serikali yake katika kulinda Uhuru kamili wa Taifa dhidi ya mienendo inayoweza kuchochea chuki na kuhatarisha amani na mshikamano iliodumu nchini wakati wote.

Tamko hilo la CCM mkoa wa Iringa linakuja mapema leo kufuatia hotuba ya Rais Dkt. Samia wakati akilihutubia Taifa katika kikao chake na wazee wa mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *