Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini Upendo Wella amewataka wananchi wa eneo hilo kutojihusisha na vurugu zilizopangwa kufanywa na baadhi ya watu wasioitakia mema nchini na badala yake wawe walinzi wa amani ili kuhakikisha hakuna yoyote anayejaribu kuvuruga hali ya utulivu wa nchi.