Rais wa Benin, Patrice Talon, ameonekana kwenye televisheni kwa mara ya kwanza baada ya jaribio la mapinduzi la Jumapili, akisema hali sasa iko shwari na waliojaribu kumpindua wataadhibiwa.

Rais wa Benin amezungumza kuwatuliza raia wa taifa hilo la Afrika Magharibi, akisema kwamba hali sasa iko chini ya udhibiti kamili kufuatia jaribio hilo, huku akilipongeza jeshi la taifa hilo kwa kutimiza wajibu na kuendelea kuwa waaminifu.

Jaribio hili la mapinduzi lililozimwa linaongeza wasiwasi kwenye eneo la Afrika Magharibi, ambalo hivi karibuni limekumbwa na misururu ya mapinduzi.

Benin, koloni la zamani la Ufaransa, kwa muda mrefu limechukuliwa kuwa moja ya taifa lenye demokrasia thabiti barani Afrika, hata hivyo Rais Talon amekuwa akikabiliwa na tuhuma za kukandamiza wakosoaji wa sera zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *