Taasisi ya Kampeni ya Kitaifa ya Mama Asemewe chini ya Uongozi wa Mwenyekiti wake Bw. Geofrey Kiliba imelaani Vikali matukio ya uvunjifu wa amani yaliyofanyika wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, suala ambalo lilivuruga shughuli za kijamii na kusababisha madhara kwa watu na mali binafsi na za umma.

Kauli hiyo imetolewa mbele ya wana habari Jumapili Disemba 07, 2025 Jijini Dar Es Salaam na Bi. Anna Abraham Kivuyo, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Mama Asemewe, akisema kuwa matukio ya Oktoba 29, yameonesha dhahiri kuwa Watanzania hawapaswi kutoa nafasi kwa matukio yanayokiuka sheria na kuathiri usalama wa umma nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *