Ghana jana Jumatano kile ilikosoa kile ilichokitaja kuwa vitendo vya “kinyama” walivyotendewa raia wa nchi hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) baada ya wasafiri kadhaa wa Ghana kuzuiliwa au kufukuzwa .

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ghana imearifu kuwa raia wao waliokuwa safarini Israel walilengwa kwa makusudi na kufanyiwa ukatili na mamlaka za Israel tangu Jumapili iliyopita na kwamba watu saba, ikiwa ni pamoja na ujumbe wa bunge la nchi hiyo wa watu wanne, walizuiliwa bila sababu “zinazokubalika” na baadaye wakaachiwa baada ya jitihada za kidiplomasia za masaa kadhaa.  

Israel pia iliwafukuza raia wengine wa watatu wa Ghana. Ujumbe huo wa bunge la Ghana ulielekea Israel kwa minajili ya kushiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Usalama wa Mitandao huko Tel Aviv; na raia wa watatu wa Ghana waliofukuzwa na Israel walirejea nyumbani kwa kutumia ndege iliyokuwepo. 

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Ghana imebainisha kuwa: Vitendo hivyo vya Israel ni vya uchochezi mkubwa na havikubaliki”

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ghana jana hiyo hiyo iliwaita maafisa wa ubalozi wa Israel huko Accra ili kueleza malalamiko yake kuhusu mienendo isiyo ya kibinadamu waliyofanyiwa raia wa Ghana huko Tel Aviv. 

Wizara hiyo imesema madai ya serikali ya Israel kwamba ubalozi wa Ghana ulishindwa kushirikiana katika kuwafurusha raia wake “hayakubaliki na kwamba ” na ubalozi huo Tel Aviv ni sikivu na unafungamana na sheria za kimataifa.

Ghana na Israel zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia baada ya nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1957. Ghana, pamoja na nchi nyingine za Kiafrika, zilikata uhusiano wao na Tel Aviv.kufuatia Vita vya Waarabu na Israel mwaka 1973. Hata hivyo, uhusiano huo ulirejeshwa katika hali ya kawaida mwaka 1994.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *