
Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amekosoa na kulaani waziwazi vitendo haramu vya Marekani katika eneo la Karibi, akisema: “Kitendo cha serikali ya Marekani cha kutuma meli za kivita huko Karibi na pwani ya Venezuela, kwa visingizio vya uwongo, ni haramu, ukiukaji wa sheria za kimataifa na ni uzushi hatari unaotishia amani na usalama wa dunia.”
katikak mazungumzo yao ya simu, Pezeshkian na Nicolas Maduro wamebadilishana mawazo kuhusu ushirikiano wa pande mbili na kujadili matukio ya hivi karibuni katika eneo la Karibea.
Pezeshkian amesisitiza uungaji mkono wa Iran kwa uhuru, usalama na utulivu wa Venezuela.
“Tunafuatilia kwa karibu matukio ya eneo la Karibi na harakati za Marekani, na tunatangaza mshikamano wetu kamili na serikali na watu wa Venezuela,” amesema Rais Pezeshkian.
Ameashiria mfungamano mkubwa wa mataifa mawili ya Iran na Venezuela na kutilia mkazo umoja wa kimkakati na urafiki wa kudumu kati ya Iran na Venezuela.
“Iran inaiona Venezuela kama rafiki na mshirika wa kweli na inaiunga mkono katika hali zote, hasa katika hali nyeti ya sasa,” amebainisha.
Rais Pezeshkian ametangaza utayarifu wa Iran kupanua ushirikiano na Venezuela katika nyanja zote, akieleza kuwa Tehran inathamini uungaji mkono wa Caracas katika majukwaa ya kimataifa.
Ameongeza kuwa: “Nina imani kwamba umoja na utashi wa kitaifa wa watu wa Venezuela vitasaidia nchi hiyo kukabiliana na changamoto zilizopo.”
Kwa upande wake, Nicolas Maduro ameishukuru Iran kwa uungaji mkono wake wa kudumu kwa serikali na watu wa Venezuela.
“Mataifa yetu yameungana kwa miaka mingi, na kwa kuanzisha uhusiano imara, yameweza kutoa mfano wa uhusiano wa kirafiki kwa amani, ushirikiano, na maendeleo,” amesema Rais Maduro.
Akizungumzia mvutano unaoongezeka katika eneo la Karibi, Maduro amekosoa vitendo vya Marekani akivitaja kuwa ni “vya uchochezi, visivyo vya lazima na kinyume na Mkataba wa Umoja wa Mataifa.”
Amesema: “Madai ya uongo ya Marekani dhidi ya watu watukufu wa Venezuela yamepingwa na maoni ya umma duniani, hata ndani ya Marekani.