Wanaharakati wa haki za kibinadamu na watafiti mbalimbali wameituhumu Benki Kuu ya Ufaransa kwamba ilihusika kwa namna moja katika matukio yaliyopelekea kutokea mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda dhidi ya jamii ya Watutsi.

Madai hayo yamewasilishwa na wanasheria Matilda Ferey na Joseph Breham kwa niaba ya Dafroza na Alain Gauthier pamoja na taasisi ya CPCR.

Watafiti waliopitia kumbukumbu mbalimbali wanadai kuwa benki hiyo iliwezesha kufanyika miamala kadhaa ya fedha kwa ajili ya serikali ya Rwanda mwanzoni mwa miaka ya 1990, ikiwa ni maandalizi ya mauaji hayo ya kimbari.

Kwa mujibu wa wasilisho hilo, inawezekana benki hiyo ilishindwa kuzuia au ikaendelea kuidhinisha pesa, licha ya tahadhari kadhaa zilizotolewa na jumuiya mbalimbali za kimataifa kuhusu mzozo wa Rwanda.

Malalamiko hayo yameegemea zaidi kwenye miamala saba iliyofanywa kutoka kwenye akaunti ya Benki ya Taifa ya Rwanda, iliyofanyika kati ya mwezi Mei na Agosti 1994.

Miamala hiyo inakadiriwa kufikia dola za Kimarekani 570,942, ambazo zinadaiwa kutumika kununua vifaa vya kijeshi na silaha, licha ya zuio la Mei 17, 1994 lililotolewa na Umoja wa Mataifa…/

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *