Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga, ameonesha kutoridhishwa na maendeleo duni ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara 13 na madaraja katika maeneo mbalimbali ya mji huo, unaotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 14.

Amesema hadi sasa mradi huo umefikia asilimia tano pekee ya utekelezaji, hali isiyoendana na thamani ya fedha iliyotengwa pamoja na ratiba ya kazi.

Mradi huo ulianza kutelekezwa mwezi Julai 2025, huku ukitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Oktoba 2026.

✍Rehema Evance
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *