Wakazi wa Kijiji cha Lowe, kilichopo Wilayani Sumbawanga, wameiomba Serikali kuwajengea daraja la kudumu litakalounganisha kijiji hicho na maeneo ya jirani, wakisema changamoto hiyo ni ya muda mrefu na imekuwa ikihatarisha usalama wao pamoja na kuathiri shughuli zao za kila siku za kiuchumi.
Wakazi hao wamesema kuwa kutokana na umuhimu wa eneo hilo kama njia muhimu ya mawasiliano na usafirishaji, walilazimika kuchangishana Shilingi milioni tisa kutoka mifukoni mwao na kujenga kivuko kwa nguvu zao wenyewe. Hata hivyo, kivuko hicho hakikidhi viwango vya usalama, hususan wakati wa mvua za masika, hali inayoongeza hatari kwa watumiaji wake.
Wameiomba Serikali kuingilia kati na kujenga daraja la kisasa litakalohakikisha usalama wa wananchi na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika eneo hilo.
✍Sammy Kisika
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates