
Israel imesimamisha shughuli za mashirika ya kimataifa 30 ya masuala ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza. Waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu wamekosoa na kulaani vikali hatua hiyo ya utawala wa Kizayuni.
Max Blumenthal mwandishi habari wa Kimarekani ambaye pia ni mhariri wa The Grayzone amesema Israel inatumia vigezo vipya vya usajili kupiga marufuku karibu kila shirika la kimataifa la misaada linaloaminika katika Ukanda wa Gaza.
Max pia ametahahdrisha kuwa hatua hiyo ya Israel itashadidisha kampeni ya kuwanyima Wapalestina, chakuka, dawa za matibabu na mahitaji mengine muhimu.
Mwandishi huyo wa Kimarekani ameongeza kuwa: Hiyo inayojulikana kama Wizara ya Israel inayohusika na masuala ya Diaspora ambayo amesema kuwa ina uhusiano wa karibu na shirika la ujasusi la Israel (Mossad) inawataka wafanyakazi wa mashirika na taasisi za misaada wathibitishe kuwa hawapingi sera za kisiasa na kijeshi za Israel wala kuhoji simulizi rasmi za Israelkuhusu vita vya mauaji ya kimbari ya utawala huo dhidi ya Gaza.
Max Blumenthal ameeleza haya baada ya Israel kuyasimamisha mashirika ya kimataifa ya misaada ya kibiandamu 37 huko Gaza. Mashirika hayo ni pamoja na Jumuiya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), CARE, Aation Against Hunger, Caritas n.k.
Wizara hiyo ya utawala wa Kizayuni inayohusika na masuala ya Diaspora imedai kuwa mashirika hayo yameshindwa kufungamana na sheria mpya za usajili zinazojumuisha kukaguliwa wafanyakazi na kuwasilisha taarifa za mtu binafsi kwa ajili ya kuajiriwa.