
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake ya kuuaga mwaka 2025 na kukaribisha 2026, amewataka Watanzania Watanzania wanapoendelea kujenga taifa lao wasikubali kugawanyika kiitikadi au kimtazamo, akirejeleamatukio yaliyotokea siku ya uchaguzi wa oktoba 2025 ambapo Tanzania ilipita nyakati ngumu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais Samia Suluhu Hassan ameuanza mwaka mpya wa 2026 kwa msisitizo wa maridhiano ya kitaifa, akitangaza maandalizi ya Tume ya Maridhiano, kuhimiza umoja, kusimamia uchumi na kukabiliana na changamoto za maji na tabianchi.
Akihutubia taifa kutoka Tunguu, Zanzibar, Rais Samia alisema serikali imeanza rasmi maandalizi ya kuunda Tume ya Maridhiano ya Kitaifa itakayohusisha wadau wote muhimu nchini.
“Nitoe rai kwenu ndugu zangu watanzania tusikubali tofauti za kiitikadi au mtazamo zitugawe na kutupotezea malengo yetu ya maendeleo na ustawi wa taifa letu.’’
“Tunapouanza 2026 serikali imejipanga kujenga umoja wa kitaifa nchini, hatua za kuunda tume ya maridhiano zimeanza kuchukuliwa,serikali itashirikiana na wadau wote katika kukubaliana kuhusu muundo wa tume,aina ya wajumbe,majukumu yao na muda wa kazi wa tume hiyo.”
“Mwaka 2025 pamoja na mafanikio makubwa tuliyoyapata,tulipitia pia changamoto na mitihani iliyotugusa sote,mtakumbuka kuwa mwezi Oktoba mwaka huu tulipitia nyakati ngumu zilizohitaji Subira mshikamano na uzalendo.”
Rais Samia alikiri kuwa kipindi kilichoelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 kilikuwa kigumu kwa Watanzania wengi, kikishuhudia mvutano wa kisiasa na maandamano yaliyosababisha maafa makubwa katika baadhi ya maeneo ya nchi.
Akihitimisha hotuba yake, Rais Samia aliwahimiza Watanzania kuukaribisha mwaka 2026 kwa mshikamano, nidhamu na dhamira ya pamoja ya kulijenga taifa.