#HABARI: Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kumkamata Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro pamoja na mke wake na kudai kuwa tayari wamesafirishwa nje ya nchi hiyo. Huku pia akidai kuwa maelezo zaidi yatafuata.

“Marekani imefanikiwa kutekeleza shambulio kubwa dhidi ya Venezuela na kiongozi wake, Rais Nicolas Maduro, ambaye yeye pamoja na mke wake wamekamatwa na kusafirishwa nje ya nchi,” aliandika kwenye mtandao wa Truth.

“Operesheni hii ilifanywa kwa ushirikiano na vyombo vya utekelezaji wa sheria vya Marekani. Maelezo zaidi yatafuata. Kutakuwa na mkutano na waandishi wa habari leo saa 11:00 asubuhi, katika Mar-a-Lago,” aliongeza.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *