#HABARI: Waasi wanaohusishwa na Kundi la Islamic State wameua takriban watu 15 katika vijiji vitatu Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, maafisa wa eneo hilo wamesema.

Mashambulizi hayo yalitokea usiku wa Alhamisi katika Wilaya ya Lubero, mkoani Kivu Kaskazini, yakilenga zaidi raia.

Kundi la Allied Democratic Forces (ADF), lililoanza kama waasi nchini Uganda lakini baadaye kujikita katika misitu ya mashariki mwa Congo tangu mwishoni mwa miaka ya 1990, linatambuliwa na Islamic State kama tawi lake.

Kwa mujibu wa Macaire Sivikunula, mkuu wa eneo la Bapere ambako vijiji vilivyoshambuliwa vipo, raia tisa waliuawa katika Kijiji cha Kilonge, raia wawili katika Kijiji cha Katanga, huku raia wawili na wanajeshi wawili wakiuawa katika Kijiji cha Maendeleo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *