Miezi 10 ya ‘hatihati’, mateso, kuwindwa na kukosa uhakika wa kuiona kesho katika kila iliyoitwa ‘leo’ imefikia tamati na hatimaye Juma Maganga, dereva wa malori ya masafa marefu aliyehukumiwa kifungo gerezani nchini Sudan Kusini amerejea nyumbani.
Katika mahojiano maalum na Azam TV, Maganga anasimulia mapito yake tangu ilipotokea ajali ya barabarani na kutiwa hatiani kwa kumgonga na kumsababishia kifo mwanajeshi wa nchi hiyo na kusota hadi kulipa faini ya zaidi ya dola za Marekani 18,000 na kuachiwa huru.
Mhariri @moseskwindi