Ripoti kadhaa kutoka vyombo vya ndani na nje zimemeripoti kuhusiana na mlipuko katika sehemu mbalimbali za jiji la Caracas, ikiwemo kambi za kijeshi.

Mashuhuda wanasema kwamba uwanja wa ndege wa kijeshi La Carlota, ulioko katikati ya jiji, pamoja na kambi kuu ya kijeshi ya Fuerte Tiuna, uliguswa na mlipuko huo unaoelezwa ni mashambulizi makubwa, na video zinazozagaa mtandaoni zinaonyesha milipuko katika maeneo yote mawili.

Sehemu kadhaa za jirani sasa hazina umeme, na ripoti zisizo rasmi zinasema ndege zimeonekana zikiruka juu ya jiji. Tukio hili linafanyika wakati ambapo mvutano kati ya Marekani na Venezuela uko katika kiwango cha juu, huku Washington ikiendelea na mashambulio dhidi ya boti za haraka katika bahari ya Carribean, ambazo inadai zinabeba dawa za kulevya.

Marekani inasema Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, hakuingia madarakani kwa njia halali na anahusika moja kwa moja na biashara ya dawa za kulevya nchini humo. Serikali ya Venezuela inasema hatua za hivi karibuni za Marekani ikiwa ni pamoja na kukamata meli za mafuta ni jaribio la kumfanya Rais Maduro aondolewe madarakani na kudhibiti rasilimali za mafuta za nchi hiyo.

Maafisa wa serikali ya Trump wameripotiwa kuwa wamepokea taarifa za mlipuko na kuhusu ndege zilizorandaranda katika anga ya Caracas asubuhi ya Jumamosi, Tukio hili linaongeza shinikizo lililokuwepo kwa Maduro baada ya wiki kadhaa za malalamiko na mashinikizo kutoka kwa utawala wa Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *