Rais Bola Ahmed Tinubu wa Nigeria ameviagiza vikosi vya usalama kuwasaka na kuwakamata waliohusika na shambulio la Kasuwan Daji katika jimbo la Niger na kuwafikisha mahakamani mara moja.
Pia aliagiza kuokolewa kwa haraka kwa waathiriwa wote waliotekwa nyara.
Maagizo ya rais ya Jumapili yanakuja kufuatia mauaji ya wanakijiji katika Jimbo la Niger.
Takriban, watu 30 waliuawa katika shambulio hilo na wengi kutekwa nyara.
Ofisi ya rais ilisema shambulio hilo lilitekelezwa na “magaidi wanaoshukiwa kukimbilia Sokoto na Zamfara baada ya shambulio la anga la Marekani kmkesha wa Krismasi.”
Rais Tinubu alituma rambirambi zake kwa familia za waathiriwa, na pia kwa serikali na watu wa Jimbo la Niger.