Wakati watu wengine wakisherehekea ndoa zao kuimarika, jijini Tanga kumeshuhudiwa tukio lisilo la kawaida lililozua hisia tofauti.

Mwanamke anayejulikana kwa jina la Zainaji Kombo, mkazi wa Majengo, ameandaa sherehe maalum ya kusherehekea kuachwa na kupewa talaka, tukio alilolipa jina la Usiku wa Talaka Maarufu ‘Talaka Ngijangija.”

Sherehe hiyo iliwakutanisha ndugu, jamaa na marafiki, ikiwa na mbwembwe, vifijo na shamrashamra, huku wageni wakishiriki kuchangia na kushuhudia tukio hilo la kipekee.

Tukio hilo limeibua mjadala mpana, baadhi wakiliona kama mwanzo mpya wa maisha, huku wengine wakiliona kama kinyume na maadili ya jamii.

✍Mariam Shedafa
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *