“Mimi ni mwalimu wa watoto wenye mahitaji maalum wenye ulemavu wa akili. Nimesoma chuo kikuu cha Dodoma. Shahada yangu ya elimu katika elimu maalum.
“Nilipomaliza chuo Dodoma niliajiriwa Serikalini. Nilikuwa nafundisha shule ya msingi Kaloleni Jijini Arusha. Kuna kitengo cha watoto wenye ulemavu wa akili
.Unajua kila binadamu kuna namna ambavyo ameitwa kwa hiyo mimi nilijikuta wito wangu upo kwenye masuala ya elimu.
“Tangu nikiwa chuo kwenye magroup nilikuwa nazungumzia sana ishu za kielimu. Nilikuwa najiita Profesa Magoda. Baadae nilijiita Mwalimu Magoda. Kuanzia hapo nilianza kuandika vitabu vinavyohusiana na masuala ya elimu”- @mwl.magodajr, Mwalimu
#LiveonClouds360
#LainiYawana
#Clouds26Nyoosha