Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano, Rahma Kisuo, amesema Serikali itaendelea kusimamia uwekezaji katika miradi yenye tija inayozalisha ajira kwa vijana, kuimarisha hifadhi ya jamii na kuongeza ushindani wa uchumi wa Taifa.
Akizungumza jijini Arusha, Kisuo ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo Mount Kilimanjaro International Convention Centre na mradi wa nyumba za makazi wa Oloirien, akisisitiza miradi hiyo itoe kipaumbele cha ajira kwa vijana.
Amesema uwekezaji huo unapaswa kusimamiwa kwa umakini ili kulinda fedha za wanachama na kuchangia kikamilifu maendeleo ya Taifa, huku akihimiza mradi wa MK-ICC kutangazwa kimataifa ili kuvutia wateja wa ndani na nje ya nchi na kuhakikisha mapato endelevu.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates