Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika sekta ya elimu inayojenga umahiri, ujuzi na maadili ili kuwaandaa vijana wenye uwezo wa kufikiri, kubuni na kufanya kazi kwa vitendo kulingana na soko la ajira.
Ameyasema hayo wakati akizindua Skuli ya Sekondari Chukwani katika maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayoendelea visiwani humo.
Amesisitiza kuwa ujenzi wa miundombinu ya elimu na maboresho ya mitaala ni mkakati wa kukuza rasilimali watu na kuharakisha maendeleo ya taifa.
Naima Haji