Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imesema itachukua hatua kali dhidi ya watu wote wanaojihusisha na vitendo vya udanganyifu katika utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa njia zisizo halali. Hatua hiyo inalenga kuziba mianya yote ya ujanja ujanja katika utoaji wa nyaraka hizo muhimu za utambulisho.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Juma Homera, mkoani Morogoro wakati wa ufunguzi wa Kliniki ya Huduma za Msaada wa Kisheria, iliyolenga kutoa elimu kwa wananchi kuhusu haki zao na taratibu mbalimbali za kisheria. Waziri Homera aliwasihi wananchi kuwa makini na kuhakikisha wanapata huduma za vyeti vya kuzaliwa kupitia mifumo rasmi ya serikali ili kuepuka kudanganywa.

#Kilichoborakabisa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *